Na Lucas Mboje, Dodoma

VYAMA vya ushirika nchini vimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya ushirika mara kwa mara kwa wanachama wake ili kujenga uelewa wakutosha kuhusu sheria, kanuni na masharti mbalimbali ya ushirika.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sita wa mwaka wa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa ametoa rai hiyo kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwani ni muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Amesema kuwa elimu ya ushirika isitolewe tu kwa watendaji na viongozi wa chama bali itolewe kwa wanachama wa ushirika ili wajue uendeshaji wake na kunufaika na huduma zitolewazo na chama. “Vyama vingi vya ushirika hapa nchini vimekufa kwa kukosa elimu ya ushirika, niwaombe sana wasimamizi wa ushirika muendelee kutoa elimu kwa wanachama”. Amesisitiza Kaimu Mrajis Chilewa.

Aidha, Kaimu Mrajis Chilewa amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria ya ushirika pamoja na kuheshimu na kusikiliza maoni ya wanachama kwani wao ndo wenye mali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Meza Kuu wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu akitoa hoja ya kuthibitisha notisi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa.  
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...