Kwa
masikitiko makubwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo anatangaza kifo
Cha Dada yake mpendwa marehemu Mwajuma Gambo kilichotokea jana tarehe
04/10/2018 kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam.
Kwa mujibu wa Mhe. Gambo, Mazishi
yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (kesho) tarehe 06/10/2018 Saa 6
Mchana kwenye makaburi ya MCHIKICHINI Ilala Dar Es Salaam.
Msiba upo nyumbani kwao Kariakoo mtaa wa Muheza Karibu na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN
Bi. Mwajuma Gambo enzi za uhai wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...