Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Kagera wanatarajia kutoa huduma ya kliniki ya Moyo inayotembea (Cardiac Mobile
Clinic) katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 11 Novemba, 2018.
Huduma tutakazozitoa ni pamoja na upimaji wa vihatarishi vya Magonjwa ya Moyo,
ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, na kutoa rufaa kwa wananchi
watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitajika kupewa rufaa kuja kwenye Taasisi
yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.
Matibabu ya kliniki ya moyo inayotembea ni matibabu endelevu yanayolenga
kuhakikisha kuwa wagonjwa wa Moyo waliopo mikoani wanapata huduma bora ya
matibabu ya Moyo na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo.
Wananchi wote wa Mkoa wa Kagera pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ili muweze kupata huduma za uchunguzi
za matibabu ya Moyo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...