Majaji
wa shindano la Fiesta Super Nyota 2018 mkoani Rukwa, wakiongozwa na
Jaji Mkuu, Adam Mchomvu (mwenye miwani), wakijitambulisha mbele ya
washiriki na wageni mbalimbali waliofika kushuhudia kupatikana wa nyota
wapya wa muziki wa kizazi kipya. wengine toka kulia ni Afisa Michezo
Manispaa ya Rukwa, Adam Evarist, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Rukwa,
Charles Kiheka na kushoto ni The Baton A ambaye alikuwa mshindi wa Tigo
Fiesta Supa Nyota mwaka jana.
Washiriki
wakiwa kwenye mchujo wa mwisho uliotoa washindi wawili ambao watapanda
kwenye jukwaa la Tigo Fiesta kesho uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga
na kupata mshindi mmoja.
Moja
kati ya washindi wawili wa Tigo Fiesta Supa Nyota mkoani Rukwa, Robby
Gitaa akionyesha uwezo wake wa kuimba na kupiga gitaa kwenye shindano la
kutafuta vijana wenye vipaji vya muziki mkoani humo leo.
Moja
kati ya washindi wawili wa Tigo Fiesta Supa Nyota mkoani Rukwa, Tigani
Tozi akionyesha uwezo wake wa staili ya kufokafoka kwenye shindano la
kutafuta vijana wenye vipaji vya muziki mkoani humo leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...