Na.Alex Sonna,Dodoma

Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto ametembelea eneo la mji wa Serikali kwa dhumuni la kuona maendeleo ya ujenzi wa miondombinu pamoja na kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi huo, jiji Dodoma.

Akizungumzia ziara ya balozi huyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwini Kunambi, amesema kuwa zaidi ya mabalozi 20 wameshafika Dodoma kujionea maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zao.

“Balozi wa Japan amekuja kuona eneo ambalo ubalozi wa nchi yake utajengwa, pamoja hilo amekuja miondombinu ambayo inaendelea kujengwa," ameeleza Kunambi.Aidha Kunambi amesema kuwa Jiji la Dodoma lipo kwenye ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi huo utakamilika Januari mwakani kwa lengo la kusambaza maji kwenye eneo la mji wa serikali kabla ya kufikiwa na miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi ya Jiji la Dodoma (DUWASA).Mkurugenzi huyo aliwahakikishia watumishi wanaohamia Dodoma kuwa huduma muhimu zinapatikana ikiwemo maji kwani wanazalisha lita 61,000 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita 48,000.
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi alipotembelea ofisini kwake kabla hajaenda kukagua eneo ambapo zitajengwa ofisi za ubalozi wa Japan
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akiangalia mchoro wa ramani wa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Ubalozi wa Japan Mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisisitiza jambo kwa Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kufanya ziara ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma Balozi wa Japan akiwa na Mkurugenzi wanaelekea katika kupanda gari 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...