Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini Tanzania ya Mwaka 2017 (THDR) inayozungumzia “Sera ya Kijamii Katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi”, ina mchango mkubwa katika kuchambua masuala yanayohusu maendeleo ya binadamu na nafasi yake katika uandaaji wa mipango ya maendeleo, utengenezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa uzinduzi wa ripoiti hiyo mjini Dodoma jana.
“Kwa mtazamo wangu, dhana hii ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi sio tu kwamba ni dhana sahihi bali pia inaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 – 2020/21.’ Alisema Dk. Mpango .
Aidha, alisema dhana ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi ni dhana ambayo imekuwa ikizingatiwa katika mipango ya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja pamoja na miongozo ya uandaaji wa bajeti za serikali.
Dk. Mpango alisisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi, kutokuacha mtu yeyote nyuma katika mchakato wa maendeleo na kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya uchumi, serikali ya Tanzania imetoa umuhimu mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ili kuinua hali za watu wake.
Waziri Mpango alisema kwamba sekta ya afya, elimu na miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ni sehemu ya juhudi zinazofanya kuwezesha uchumi jumuishi.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu
Kazungu (wa nne kulia) akikata utepe kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square
mjini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie
Bouckly, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya (kulia) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya
Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa tatu kulia).
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu,
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu pamoja na
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius
Ruyobya katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala ya Ripoti
ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya
kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu
Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya
wizara hiyo Dkt. Phillip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti
ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika
ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini
Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni
waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu
ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa
Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie
Bouckly ambao ni wafadhili wa ripoti hiyo akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu
ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa
Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kulia ni Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
Wadau
kutoka taasisi mbalimbali za serikali bara na visiwani, ESRF, Umoja wa
Mataifa pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma walioshiriki kwenye
hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR)
ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo
la Treasury Square mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...