Sekta ya afya inakua kwa kasi huku huduma muhimu za afya kwa sasa zikiwa zinapatikana hapa hapa nchini”

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alipokua akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro jana Novemba 22, 2018.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Sekta ya Afya imepewa kipaumbele cha hali ya juu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu mageuzi makubwa ndani ya sekta ya afya yameanza kuonekana huku huduma za matibabu ya kibingwa yakiwa zikipatikana hapa hapa nchini.

“Tunasimama hapa kifua mbele tukiona mabadiliko katika hali ya upatikanaji wa dawa kuimarika zaidi, bajeti ya dawa imeongezeka toka Shilingi Bilioni 30 mpaka Shilingi Bilioni 270 yaani mara tisa zaidi ndani ya miaka mitatu” alisema Mhe.Naibu Waziri na kuendelea “Tumeboresha vituo vya afya takribani 300, huku Mkoa wa Kilimanjaro ukiwa na Vituo 8 vilivyoboreshwa vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 na kwa mwaka huu 2018 Serikali imeanza kujenga Hospitali za Wilaya 67 nchini”

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya Hospitali mpya za Rufaa za Mikoa ili ziweze kutoa huduma za kibingwa, kupunguza msongamano wa wagonjwa na ucheleweshwaji wa huduma katika Hospitali za rufaa za kanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisoma nyaraka za matibabu za Bi. Mary Nyange (kulia) anayepatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua benki ya damu zilizopo katika jokofu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...