Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akijibu maswali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb).

Dkt. Ndumbaro alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Ndumbaro akijibu swali kuhusu sababu zinazofanya hadi sasa Tanzania kutoridhia Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora uliopitishwa mwaka 2017.Mhe. Naibu Waziri alieleza kuwa Tanzania inachelewa kuridhia kutokana na baadhi ya ibara za mkataba huo kukinzana na Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani). 
Dkt. Ndumbaro akiendelea kujibu maswali mbalmbali ya nyongeza yaliyokuwa yakiulizwa na Waheshimiwa Wabunge. 
Mkutano wa Bunge ukiendelea 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akimpongeza Naibu Waziri, Mhe. Damas Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu Maswali Bungeni. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi akimpongeza Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu maswali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...