Na Mathias Canal-WK, Mwanza

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewapongeza wakuu wa mikoa yote nchini inayozalisha pamba, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa usimamizi bora uliopelekea uzalishaji wa zao hilo kuwa maradufu katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/2019.

Dkt Tizeba ametoa pongezi hizo leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018 wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza na kusema kuwa Uzalishaji wa pamba katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/19 umeongezeka kwa asilimia 67 kutoka tani 133,000 hadi tani 221,600. 

Pamoja na pongezi hizo waziri huyo amewataka viongozi hao kuongeza ufanisi wa usimamizi wa zao hilo kwani pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji lakini bado matarajio ya uzalishaji hayakufikiwa kwa mujibu wa makubaliano.

Alizitaja sababu zilizopunguza uzalishaji kuwa ni pamoja na Ukame mkali kati ya mwezi Januari na Februari ulipukutisha vitumba vichanga; Mripuko wa wadudu wakiwemo viwavi jeshi vamizi, vidung’ata, chawa jani, vithiripi, vidukari. Wadudu wanaofyonza miaka ya nyuma halikuwa tatizo kwenye pamba; Mvua kubwa kupita kiasi kati ya Machi na Mei ilizamisha pamba kwenye maeneo yote ya mbuga na mabondeni; sambamba na Ufahamu mdogo wa wakulima kuhusu matumizi ya viuadudu. 

Alisema, mfumo wa kuzalisha mbegu bora za pamba umefufuliwa na unafanya kazi. Mbegu mama (Breeder seed) inazalishwa katika Taasisi ya Utafiti ya Ukiriguru na inakwenda kupandwa katika shamba la Nkanziga lililopo Wilayani Misungwi ili kuzalisha (Prebasic seed)
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Shinya Mhe Zainabu Telack, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri wakifatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) Ndg Japhet Justine akifuatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dkt Joel Kabisa akizungumza wakati wa mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...