Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka askari pamoja na watumishi mbalimbali waliopo ndani ya Wizara yake wawe huru kuuliza maswali, kusema kero zao zinazowakabili katika vikao vyake na hakuna kiongozi yeyote atakaye wanyanyasa baada ya yeye kuondoka.

Waziri Lugola amesema hayo baada ya kuona baadhi ya watumishi katika ziara mbalimbali anazozifanya nchini, wanakua na woga wa kusema kero zao wakihofia watapata matatizo baada ya yeye kumaliza kikao. , wakati anapata mambo mengi ambayo yanamsaidia kutatua kero za watumishi wake licha ya kuwa baadhi ya watumishi wanakua na woga wa kusema matatizo yanayowakabili.

Akizungumza katika kikao na askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri, liliopo Wami-Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro, jana, Lugola alisema ili aboreshe utendaji kazi wa Wizara na Idara zake, anahitaji kujua matatizo mbalimbali ya watumishi wake, hivyo katika kikao chake ruksa watumishi kuuliza maswali kwasababu kupitia maswali hayo yanamsaidia sana kutatua kero zao.

“Mimi ndio Waziri wenu, ulizeni swali lolote, toeni kero zenu na hakuna wakuwafuatilia baada ya kikao hiki, hiki ni kikao cha Waziri wenu mmepata nafasi hii ulizeni, niambieni matatizo yenu yanayowakabili ili tuyafanyie kazi,” alisema Lugola. Pia aliwaambia watumishi hao endapo watapata matatizo baada ya kusema kero zao katika kikao chake, wawe huru kumuambia japo anaamini hakuna chochote kitakacho wakuta maana kikao chake ambacho ni huru.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akionyesha moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, ambayo inahitaji matengenezo. Lugolo alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo la Kilimo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni askari wa Gereza hilo, Sajenti Lubimbi Sayi. Lugola alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikikiliza Mkuu wa Gereza la Mbigiri, Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe (kulia) alipokua anatoa taarifa ya utendaji kazi wa Gereza hilo la Kilimo. Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na askari na Maafisa wa Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri lililopo Mvomero, Mkoani wa Morogoro, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto kwa Waziri huyo ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola aliwataka na askari na Maafisa hao kusema kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akichungulia ndani moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri ambayo inahitaji matengenezo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupokea kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...