Diamond Trust Bank (T) Ltd, (DTB-Tanzania) leo hii, imekabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Amana, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za kijamii. DTB-Tanzania kila mwaka hutenga asilimia 2% ya faida yake kwa ajili ya utekezaji wa shughuli za kijamii. Fedha hizi huelekezwa katika kuboresha huduma katika sekta za Afya, Elimu na Mazingira.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji. Vyote hivi vikiwa na thamani ya Tshs 10,000,000.00.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Dk.Kilomoni alishukuru uongozi wa DTB-Tanzania kwa urafiki uliopo kati ya taasisi hizi mbili ambapo kila mwaka, DTB-Tanzania hutoa msaaada kama huo kwenyeb Hospitali hiyo.

Naye Mkurugenzi wa fedha wa DTB-Tanzania, Ndg. Joseph Mabusi, akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano alisema, “kama taasisi ya kifedha kamwe hatuwezi kusahau jamii. Ni Dhahiri kwamba faida yetu hupatikana katika kufanya biashara na jamii inayotuzunguka. Kwa mtizamo huo, kila mwaka DTB-Tanzania hutenga fedha ambazo hutumika kwenye shughuli kama hii ya leo”.

Ngd, Mabusi alieleza kwamba DTB-Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo, wamekuwa wakilipa ada ya shule kwa watoto yatima watano kutoka kituo cha Kurasini katika shule ya sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha, pia wamukuwa wakichangia miche ya miti katika Wilaya ya Nyamagana -Mwanza, ikiwa na mtizamo wa kuboresha mazingira katika milima iliyoharibiwa na shuguli za kibinadamu.
Mkurugenzi wa fedha wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa tatu kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni baiskeli za wagonjwa ambapo pia walikabidhi vifaa tiba mbalimbali ikiwemo ni pamoja na magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa (wan ne kushoto) na wa wafanyakazi wa benki hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dk. Amim Kilomoni (wa pili kushoto) na Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Anna Musa (kushoto) wakisalimiana na wafanyakazi wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa pili kulia) na Sylvester Bahati (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka Benki hiyo ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa, akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa DTB Tanzania baada ya wafanyakazi hao kufanya ziara fupi katika hospitali hiyo ambapo pia walikabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...