Baadhi ya Wananchi wa mitaa ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,mjini Kibaha wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini, Silvestry Koka wakikagua kivuko mtaa wa Lumumba kuvuka mto Mpiji kwenda Kibwegere Kibamba Dar es salaam, wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

WAKAZI wa mitaa ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,mjini Kibaha wameanza kujitolea kujenga kivuko cha muda kuvuka mto Mpiji ili kuepukana na maafa ya kujeruhiwa na mamba kutokana na kero kubwa ya ukosefu wa kivuko cha kudumu. Kufuatia jitihada hizo ,mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka amechangia milioni tatu ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.

Akikagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho kuvuka mto kwenda Kibwegere Kibamba Dar -es salaam, wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo, Koka alisema wakati wakielekea kwenye mkakati mkubwa ,hakuna budi kuanza na mkakati wa muda mfupi.Alibainisha ,serikali kupitia wakala wa barabara mijini( TARURA )imetenga sh.mil 500 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko hicho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kujenga kivuko kikubwa na cha kudumu .

"Nilipiga kelele kuhusu kivuko hiki na kimeitikiwa na TARURA kuna mpango wa kujengwa ambapo imeshatengwa mil 500 ila tatizo lililopo ni mvutano kati ya TARURA Kibamba na Kibaha,jambo ambalo linafanyiwa kazi  ".
Mbunge Wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka (wa pili kulia) akizungumza wakati alipokwenda kukagua kivuko mtaa wa Lumumba kuvuka mto Mpiji kwenda Kibwegere Kibamba Dar -es salaam ,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo ,wa kwanza kulia mwenyekiti wa ujenzi Jerome Munisi.

" Nia yangu ni kuona kivuko cha kudumu ila wakati mambo hayo yakiendelea kufanyiwa kazi ,nawaomba mhusishe wataalamu katika harakati hizi ili kuondokana na hasara ya kujenga kisha kivuko kusombwa na maji ya mvua mara kwa mara ,

"Kipindi cha nyuma nilishatoa milioni nne kwenye kivuko ambacho kilisombwa na mvua kubwa iliyonyesha ,sasa inahitajika milioni 28 kukijenga kingine,mimi nachangia milioni tatu tena"alifafanua Koka.

Mwenyekiti wa mradi huo ,Jerome Munisi alisema wameungana mitaa ya Lumumba ,Muheza na Kibwegere (LUMUKI)kukabiliana na tatizo hilo baada ya watu kujeruhiwa na mamba. Alielezea, mchango wa kaya wametoa mil 3.9,kanisa katoliki 530,000,chemchem ya uzima 750,000 jumla mil. 5.250 hivyo kwasasa mahitaji ya mafundi bado ni milioni 20 ambazo zitasaidia kujenga kivuko hicho.
Mkazi wa Lumumba Frenk John ,aliomba jitihada ziongezwe kwa kuitisha mkutano utakaolenga kuhamasisha wananchi kujitolea kujenga kivuko cha muda ili kuondokana na adha zilizopo kabla ya mvua kuanza. Hata hivyo ,Koka alikagua kivuko kingine cha Mkombozi kinachojengwa kwa kushirikiana na Jeshi kwa kushirikiana na wananchi na serikali ambapo yeye alishachangia milioni 11.

Aliahidi kuendelea kuwahimiza wajenzi wa daraja ambao ni jeshi na kwamba atawasiliana na makao makuu ya jeshi ili kuweka msukumo kitako cha daraja kipelekwe kabla ya mvua kubwa kunyesha.

Pia, mbunge huyo alitembelea ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Kidimu katika kata hiyo, na kudai atahakikisha anasimamia ujenzi huo ukamilike mapema ili wanafunzi waingie mwakani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...