Takribani nchi zaidi ya 30 na washiriki wa Karate wapatao 300 ikiwemo Tanzania kuwakirishwa na sensei Fundi Rumadha Dan 4 wa chama cha Jundokan Tanzania, wamekamilisha sherehe maalum toka chama cha Jundokan kuanzishwa na master Eiichi Miyazato, baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Karate wa Goju Ryu master Chojun Miyagi sensei kufariki. Hizi ni sherehe kubwa hufanyika kila baada ya miaka mitano, zimewakusanya walimu na wanafunzi toka mabara yote, ikiwemo na Tanzania.

Sherehe hiyo inaendelea katika ukumbi maalum wa michezo ya sanaa za mapambano " Okinawa Karate kaikan Hall ", ukumbi mpya kabisa uliofunguliwa na mfalme Akihito miaka miwili iliyopita. Ukumbi huu, utakuwa umeupumzisha ule wa zamani wa " Budokan Hall".

Pia, sensei Fundi Rumadha, alipewa fursa ya kuwa miongoni mwa walimu au masensei wa nje ya Japan kufanya maonyesho ya kata mbele ya masta wa karate maarufu toka kisiwani hapo Okinawa. Pia hii ilikuwa fursa pekee kwa watu wa Okinawa kuona kwamba Tanzania inalo tawi la chama hicho na kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye sherehe hizo.
Zaidi ya hayo, sambamba na hii sherehe kubwa kisiwani hapo,  kutakuwa na mahudhurio ya makumbusho na kuona  minara ya kumbukumbu za waasisi wa mitindo mbalimbali ya Karate kwa washiriki wote.
Pia, wakati wa shughuli hizo, sensei Fundi Rumadha alipata fursa ya mahojianona gazeti la "Okinawa Times", na kutaka kujua, kuna hamasa gani na jinsi gani watanzania wanavyoona kuhusu mchezo wa Karate huko Tanzania.

Sherehe ya kufunga maadhimisho hayo zitafanyika usiku wa leo Jumapili kwa masaa ya Japan. Baada ya mitihani ya mikanda tofauti miesi ya walimu toka shule au dojo mbalimbali kumalizika asubuhi ya leo.
Sensei Rumadha (wa kwanza kushoto) na washiriki wenzie wakifanya Sachin kata. Angola na Tanzania ni moja ya nchi za Afrika kushiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sensei wangu Fundi Rumadha kuiwakilisha Tanzania nasi wana Goju ryu JUNDOKAN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...