Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na mwenzake, sababu shahidi wa upande wa mashtaka ana dharura.

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru Vitalis Peter amedai leo Novemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika Kesi hiyo amepatwa na dharura.

Kutokana na hiyo, Hakimu Simba alisema kwa mtindo huu hii Kesi haitomalizika, watakuwa wanacheza tu."Wasa muwe mnaleta mashahidi Wawili Wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea kwani hali kama hii imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne au tano" amesema Hakimu Simba.

Wakati upande wa utetezi ukiwakikishwa na Wakili Alex Mgongolwa amewataka mashahidi wanaokwenda kutoa mashahidi katika Kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta anahitilafu watafute mwingine.

Aidha hakimu Simba ameusisitiza upande wa mashtaka kupeleka mahakamani hapo mashahidi wawili wawili.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo utaendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Katika kesi hiyo, Gugai na wenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, katika Mahakama hiyo.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Gugai ni kosa la kumiliki mali zilizozidi kipato chake halali, ambapo anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2005 na Desembea 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...