Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mererani Wilayani Simanjiro.Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.

“Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.

Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Kampuni ya Godmwanga Gem Ltd Bw. Andrew Mbando (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti (kulia) wakati alipotembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mzawa kwa asilimia ambayo inachenjua madini ya Kinywe (Graphite). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka  jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...