Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Dodoma

MBUNGE wa  Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Zuberi Kuchauka amesema huu sasa ni muda wa  kufanya kazi na  kutekeleza Ilani ya Chama hicho kwa kasi  ya Rais Dk.John Magufuli katika jimbo  lake.

Kuchauka amesema hayo Mjini  Dodoma ambapo anashiriki Bunge la  11 ,kikao cha 13 mara baada ya kuapishwa kuwa Mbunge kwa tiketi ya CCM.

"Nawashukuru wananchi wa  Liwale kwa kuendelea kuniamini katika kipindi kingine nikiwa ndani ya CCM.Mnakumbuka nilikuwa upinzani na kisha kujiunga CCM na leo ni mbunge kupitia chama hicho.Nawashukuru wananchi kwa kuendelea kuniamini.

" Niwahaidi wakazi wa  Liwale kuwa sitowaangusha katika miaka miwili iliyobaki.Nitashirikiana nanyi katika kuhakikisha jumbo letu linapata maendeleo kwa kasi,"amesema Kuchauka

Amesema kuwa katika miaka hii miwili ambayo imebaki  atahakikisha anaendeleza pale alipoishia kwani uwanja ni ule ule na kilichobadilika ni timu ambayo amejiunga nayo ambayo ni sahihi kwa kuleta maendeleo ya Jimbo la Liwale.

Amefafanua  yeye ni Mbunge wa  CCM na  Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM chini  ya Rais Dk. Magufuli ambaye msimamo wake ni kusaidia watu maskini na  kuchapa kazi kwa  bidii.

Pia ameshukuru viongozi wa CCM pamoja na wananchi wote kwa kumuamini na  kurudi kugombea tena katika uchaguzi Mdogo na hatimaye kuibuka na ushindi.
MBUNGE wa  Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka  alipofanya mahojiano mafupi na Michuzi TV jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...