Na Mwashungi Tahir ,Maelezo

Mkurugenzi wa Uwezeshaji Mamlaka ya Udhibi wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Omar Zubeir Ismail alisema SeriKali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo kwa kitalu cha Pemba Zanzibar.

Hayo ameyasema leo huko Bandarini Malindi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasili meli kubwa ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kina kifupi cha maji. 

Aidha alichukua nafasi kwa kuwajuilisha wananchi kazi ya utafiti wa mafuta na gesi Asilia kwa njia ya mtetemo bado inaendelea kwa upande wa kina kifupi cha maji (TRANSITION ZONE 2D SEISMIC SURVEY) katika maeneo ya visiwa hivyo.

“Nachukua nafasi hii kuwajuilisha wananchi kwamba suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ni la muda mrefu na linaweza kufika hadi miaka kumi kukamilika nawaomba muendelee na kazi zenu za kawaida”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema tumuombe Mungu tufanikiwe suala hili kwani likifanikiwa ni la wote kwa maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu vya hapo baadae. Pia alisema meli zitakazotumika katika zoezi la mtetemo kwa kina kifupi cha maji tayari zimeshawasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo. 
Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji 
Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji. PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...