Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) limefanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

 SECAD ni mradi ambao kwa jumla utatekelezwa kwa miaka mitano ikiwa ni awamu ya kwanza na ya pili ambapo umejikita kuhakikisha wanaongeza uhifadhi wa mazingira kwa maana ya kwenye hifadhi ya Selous pamoja na ushoroba (corridor) unaounganisha pori la akiba la Selous na hifadhi ya Niassa ipatikanayo nchini Msumbiji

Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo jana kwamba ugeni wa shirika hili uliofika wilayani kwake ulitembelea na kujionea maendeleo ya mradi  na kutembelea jumuiya ya uhifadhi ya Mbarang'andu ambapo walipata taarifa ya mradi na kujionea mafanikio, mipango na changamoto kwa sasa. 

Mkuu wa Wilaya huyo ameueleza ugeni wa shirika hilo kuwa moja ya mafanikio ni mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ambao unaosimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki.

Kuhusu changamoto amesema moja ya changamoto ya mradi ni  wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji

Pia walitembelea Chuo cha Likuyu ambacho kinatumika kufundisha VGS (village scouts) wanaotumika kulinda hifadhi hizo. 
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akipewa maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa wa SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program) wakati SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) likifanya zaira wilayani yumo kufuatilia mradi huo  
 Eneo la mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akiwa sambamba na Wadau wa  SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) wakionesha chupa ya asali ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ,ambao unasimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki. 
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akikaribishwa mara baada ya kuwapokea wageni kutoka SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) llilofanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...