Na Genofeva Matemu – JKCI.

Zaidi ya watoto 750 wenye matatizo ya moyo hapa nchini wamefaidika na matibabu ya moyo kutoka kwa wataalam wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel tangu mwaka 1999.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. David Eyal alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa kutoka SACH kwa kushirikiana na JKCI.

Mhe. Naibu Balozi Eyal alisema watoto hao kutoka Tanzania Bara na Visiwani walifanyiwa uchunguzi na kutibiwa hapa nchini wale ambao walikutwa na matatizo yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu walipelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu zaidi. Gharama za usafiri na matibabu ziligharamiwa na Serikali ya Israel.

“Kujitoa kwa wataalam kutoka Shirika la SACH kuja Tanzania kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni ubalozi wa kweli wa kuitangaza nchi ya Israel kwa vitendo, ni matarajio yetu kuwa huduma hii itakuwa endelevu na kuendelea kuokoa maisha ya watoto wetu wengi zaidi”, alisema Mhe. Naibu Balozi Eyal.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongozana na mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akielekea kuangalia ukarabati wa jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiangalia kipimo kinachoonyesha jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto(Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongea na wazazi wa watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...