Na. Vero Ignatus, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameanza ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Arusha, Arumeru na Longido kukagua maendeleo ya Miradi Mikubwa ya Maji inayotekelezwa katika wilaya hizo.

Akiwa katika halmashauri ya Jiji la Arusha Gambo ametembelea mradi mkubwa wa Maji unaotekelezwa Jijini humo pamoja na baadhi ya kata za wilaya ya Arumeru.Gambo ameitaka Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafishaji Mazingira Jiji la Arusha AUWSA kuweka kipaumbele katika utunzaji wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika mlima Meru ili kuhakikisha miradi hii inayotumia fedha nyingi inakua endelevu.

“Nimewahi kusikia wataalam wa Maji wakisema Vita ya Tatu ya dunia itahusisha kugombea maji, ninaomba sisi tuanze kujihami kwa kutunza vyanzo vyetu vya maji''alisema Gambo

Ameotaka bodi ya AUWSA kuandika andiko la mradi ambalo watalipigia debe katika Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia Mazingira ili kuweza kupata ufadhili wa kampeni hiyo ya utunzaji wa Vyanzo vya Maji. "Itakua haina maana kutumia kiasi kikubwa hivi cha fedha ikiwa baada ya miaka michache ijayo vyanzo vyote vitakauka” alisema Gambo"

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wa maji utakua historia.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia moja ya Visima ambavyo ni chanzo cha Maji yanayotarajiwa kuhudumia Jiji la Arusha.
Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo ya mapito ya mtandao wa maji taka. 

Mafundi wa kampuni ya Cheil Engeneering wakiwa katika uchimbaji wa kisima kilichopo wilayani Arumeru
Miundo mbinu ya mfumo wa maji taka, mabwawa haya yanajengwa katika eneo la Terrat pembezoni mwa Jiji la Arusha. Mabwawa haya yanakadiriwa kuwa na uwezo wa kutibu takribaniita Milioni 22 kwa siku za Maji Taka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...