Na Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchini ikiwa ni juhudi za kukabiliana na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisi nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Polisi cha Songe ambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu, udogo wa majengo katika vituo mbalimbali nchini na iko katika mpango wa kujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.
“Serikali inatambua changamoto ya vituo vya polisi hasa katika wilaya mpya nchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujenga vituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu, lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukio ya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni
Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambao wako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneo nchini ambako vituo vya polisi vimejengwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi na serikali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi kuingia Kituo cha Polisi cha Songe, ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo na Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Warda Abeid.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Warda Abeid.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , Edward Bukombe, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani, ) kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...