Serikali inawataadharisha wananchi wanaoharibu miundombinu ya njia ya reli kwa kuwa imeazimia kuwachukulia hatua kwa wanaojishughulisha na shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la hifadhi ya miundombinu ya njia ya reli na kwa wanohujumu miundombinu hiyo kwa kuiba 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa miundombinu ya njia ya reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Arusha akiwa kwenye stesheni ya treni ya Mombo iliyopo mkoani Tanga .
Nditiye ameyasema hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama kuwa washirikiane na Shirika la Reli Tanzania (TRC), viongozi na wananchi wanaoishi maeneo inakopita reli hiyo na vyombo vya ulinzi na usalama kuilinda na kuitunza reli kwa kuwa reli ni uchumi na inachangia maendeleo ya taifa letu, tuilinde na tuitunze. “Ni marufuku kufanya shughuli yoyote ya kibanadamu ndani ya eneo la mita 30 kulia na kushoto mwa njia ya reli kwa kuwa kwa kufanya shughuli za kilimo au kibinadamu unasababisha udongo kuja kwenye njia ya reli na kuharibu miundombinu ya njia ya reli,” amesema Nditiye.
Pia ameongeza kuwa wapo baadhi ya wananchi wanahujumu reli yetu, wanafungua vifungashio ambapo inaweza kusababisha treni kuanguka kwa lengo la kutaka kuiba mataruma na reli yenyewe, viwanda vya chuma chakavu wafikie mahala watafute malighafi inayotakiwa.  Amesema kuwa treni ikirushiwa mawe wakati inatembea na ikitokea kioo kikapasuka, treni hiyo isimame na wananchi waishio eneo hilo wachukuliwe hatua.
Nditiye amesema kuwa hakuna Serikali makini inaweza kupuuza usafiri wa njia ya reli ambapo kwa kutambua hilo, Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano ameona afufue reli hii ambayo inatakiwa ianze kufanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018. Amefafanua kuwa reli ni usafiri wa gharama nafuu na starehe na itasaidia kuzuia uharibifu wa barabara kwa kusafirisha mizigo mizito
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa amesema kuwa watashirikiana na TRC kuhakikisha kuwa wanalinda rasilimali za reli, “reli ni rasilimali zetu,” amesema Kasongwa.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu mataruma yanayohitajika kukarabati njia ya reli ya Korogwe – Mombo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Reli wa Shirika la Reli Tanzania Mhandisi Felix Nlalio (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye ziara ya kukagua reli hiyo mkoani Tanga. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye kikoti cha njano) akipata maelezo kuhusu vifungashio vya mataruma ya reli vinavyohitajika kwa ajili ya kukarabati njia ya reli ya Dar es Salaam – Moshi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Reli wa Shirika la Reli Tanzania Mhandisi Felix Nlalio (aliyeinama) wakati wa ziara yake mkoani Tanga ya kukagua ukarabati wa reli hiyo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda  kiberenge kwa ajili ya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ya njia ya reli ya Dar es Salaam – Moshi katika stesheni ya Mombo mkoani Tanga

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...