Dar es Salaam: Novemba 5, 2018, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano na Mazingira Ndugu January Makamba wamezindua mradi utakaogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 20 ili kuboresha usimamizi katika kuhifadhi mazingira kwenye ukanda wa magharibi mwa Tanzania.

Mradi huu wa uhifadhi wa mazingira unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na utatekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja na Taasisi ya Jane Goodall (JGI).

Mradi huu mpya utasaidia watu wa Mikoa ya Kigoma na Katavi, pamoja na serikali za mitaa, katika utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi na utakaonufaisha vijiji 104.

Mradi huu wa Uhifadhi wa Mazingira umeundwa kulinda mazingira wakati pia unasaidia wananchi katika shuhuli za kujikimu kiuchumi na maisha bora kama vile uzalishaji wa kahawa na utalii asili kwa ajili ya watanzania. Taasisi ya Jane Goodall itafanya kazi kwa karibu na jamii ili kuhamasisha mazoea endelevu zaidi ya usimamizi wa ardhi na kukuza elimu ya mazingira, kwa kutumia majukwaa kama vile mradi iliyofanikiwa sana ya Roots na Shoots ya Taasisi ya Jane Goodall.

Zaidi ya hayo, kama sehemu ya ruzuku hii, Taasisi ya Jane Goodall itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuunda mifumo imara zaidi katika kuhifadhi na kulinda sokwe walioko ndani na nje ya maeneo tengefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...