Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
amerasimisha bandari bubu nne mkoani Tanga kati ya bandari bubu 48
zilizopo mkoani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo
na kupata taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Tanga. Nditiye
amerasimisha bandari bubu ya Moa iliyopo Wilayani Mkinga, Kigombe
(Muheza), Kipumbwi na Mkwaja zilizopo wilayani Pangani.
Nditiye amesema kuwa amerasimisha bandari bubu hizo nne tu kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani Tanga kwa kuwa zipo mbali na bandari ya Tanga, zipo mipakani na nchi za jirani, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuiwezesha Serikali kukusanya tozo na kodi mbali mbali kwa ajli ya kutoa huduma kwa wananchi.

“Naiagiza TPA kuhakikisha kuwa bandari bubu nne
nilizorasimisha zinafanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka
2019 na wahakikishe kuwa watumishi wa TPA na TRA wanakuwepo kwenye
bandari hizo pamoja na ofisi zote za Serikali zinazohitajika ikwemo
Jeshi la Polisi,”.
Pia ameitaka TPA kwa kushirikiana na TRA itoe elimu kwa wateja kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ya Serikali kwa kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa ni kidogo ukilinganisha na athari wanazopata wananchi na wafanyabiashara kwa kuhatarisha maisha yao kwa kukwepa kodi na kutumia bandari bubu kupitisha mizigo na bidhaa nje ya bandari rasmi zilizopo na kupita maporini.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea shukrani za Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Moa, Rambazo A. Mohamedi (wa kwanza kushoto) kwa kurasimisha bandari bubu ya Moa kuwa bandari rasmi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa bandari ya Tanga, Percival Salama
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kutoka kwa Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama (aliyesimama katikati) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua bandari hiyo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu upakuaji wa mafuta melini kutoka kwa Nahodha Andrew Matilya wakati wa ziara yake ya kukagua bandari ya Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipokea taarifa kuhusu bandari bubu ya Moa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu mkoani Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...