NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 


TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU )mkoani Pwani ,inafuatilia miradi nane yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 9.800.4 kutokana na kuitilia shaka. 

Aidha taasisi hiyo imetaja,idara zinayoongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa ,kuwa ni serikali za mitaa kwa malalamiko hasa katika mamlaka za watendaji wa vijij,mitaa na kata, ikifuatiwa na polisi.

Kamanda wa TAKUKURU mkoani Pwani, Suzan Raymond alieleza hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji katika kipindi cha miezi mitatu. Alieleza, miradi tisa ilifuatiliwa katika kipindi cha julai – septemba mwaka huu ,ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo, afya, maji na elimu. 

Susan alisema, kati ya miradi hiyo iliyofuatiliwa, miradi nane inatiliwa shaka na uchunguzi unaendelea ili ikibainika kuna mapungufu hatua zaidi zitachukuliwa. WAKATI HUO HUO katika kipindi hicho ,taasisi hiyo ilipokea malalamiko 79 kati ya hayo malalamiko 35 yanahusiana na vitendo vya rushwa na uchunguzi wake unaendelea.

Suzan alifafanua, idara inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa ni serikali za mitaa kwa malalamiko 21, ikifuatiwa na polisi 09, binafsi 08, baraza la ardhi 07, mahakama malalamiko 06, elimu 06, Afya 05, Ardhi 04, Kilimo 03, Ujenzi 02, fedha 02, TASAF 01, NIDA 01, Siasa 01, Uhamiaji 01, mali asili 01 na RITA 01. 

Kwa mujibu wa Suzan , hadi sasa jumla ya kesi 28 zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali za Pwani. Alielezea katika kipindi cha julai – septemba ,kesi nne zimeamuliwa kati ya hizo tatu zimeshinda na moja mshitakiwa ameachiwa huru. 

Kamanda huyo, ameomba ushirikiano kwa jamii katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na kuwa tayari kutoa ushahidi kwa mtu mmoja mmoja ama taasisi kwa lengo la kuthibitisha uwepo wa vitendo vya rushwa vinavyotolewa taarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...