Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa mwenyeji mazoezi ya mafunzo ya Ushirikiano Imara 2018 ya kijeshi ya vikosi vya Majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki Kuanzia Novemba 9 hadi 21 mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Mkuu wa Mafunzo na Oparesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga katika kujenga uwezo wa kukabiliana na uharibifu pamoja na majanga. 

Alisema kuwa dhumuni la zoezi hilo la kikanda ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji ikiwemo kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi nyingine. “Kutokana na Oparesheni Matumbawe iliyofanyika mwaka jana kuleta matokeo bora tumeona na awamu hii kuutumia mkoa wa Tanga kwa ajili ya mazoezi hayo ya vikosi “alisema Meja Jenerali Kapinga. 

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa ya awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni mafunzo ya ndani yameanza leo mjini hapa wakati awamu ya pili itahusisha mafunzo ya nje yatakayoanza Novemba 9 mwaka huu.Aliongeza kuwa pamoja na mafunzo hayo majeshi hayo yataweza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa jamii ya wanatanga kama vile ujenzi wa ofisi ya walimu,na vyoo katika shule ya msingi Machemba iliyoko wilayani Muheza. 

Pia alisema kuwa kutakuwa na utoaji wa huduma bure za tiba katika eneo la zoezi kwa wananchi kwa magonjwa mbali hivyo kutumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa matibabu. Nae Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa vikosi vya majeshi ya nchi za Burundi,Kenya,Uganda na Rwanda tayari vimeshawasili mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya mafunzo hayo. 

Alisema kuwa kwa mwaka huu idadi ya wanajeshi 1500 wanatarajia kushiriki katika mafunzo hayo ,kwa kupeana ujuzi na kubadilishana mbinu mbalimbali za kijeshi. “Mazoezi hayo ni fursa nzuri kwa mkoa wetu nah ii inaonyesha ni namna gani mkoa ulivyo katika hali ya usalama ,utulivu na amani ndio maana kwa mara ya pili mafunzo yanaletwa Tanga.
MKUU wa Mafunzo na Operesheni Jeshini(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga kushoto akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu kufanyika mafunzo ya Kijeshi mkoani Tanga yanayo julikiana kama “Ushirikiano Imara 2018” ambayo yatahusisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkoa huo kuwa mwenyeji wa mafunzo ya kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayoitwa “Ushirikiano Imara 018”yatakayohusisha askari 1500 kutoka nchi tano kushoto ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga
 Mkuu wa Mafunzo na Operesheni Jeshini(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...