Kampuni ya Magari ya TATA Motors kwa kushirikiana na msambazaji wake nchini Tanzania Tata Africa Holdings imezindua magari aina ya Tata HEXON na Tata HEXA ambayo na kutangaza kuyaingiza katika soko la Afrika huku mnunuzi akipewa chaguo la kuamua kulipa kidogokidogo kila mwezi.
Magari hayo ambayo yamezinduliwa India mwaka 2017 hapa Tanzania
yamezinduliwa Novemba 2.2018 na Kampuni hiyo imesema magari hayo yatakuwa yakipatikana nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kupitia kwa mawakala wao walioidhinishwa.
“Tunafurahi kutangaza uzinduzi wa gari zetu hapa nchini. Gari zote hizi zimetengenezwa kwa ubunifu, viwango bora na teknolojia endelevu. amesema Mkuu wa biashara za kimataifa wa Tata Motors, Sujan Roy.
Ameongeza, kwa uzinduzi huo wanatarajia kupanua ukubwa wa soko hapa nchini na ana imani bidhaa hiyo imeingia sokoni wakati mwafaka na wanunuaji wote watapata ofa ya bima isiyozidi Sh2.5 milioni sanjari na waranti ya miaka 3 kwa Kilimeta 60,000 tu.
Kadhalika amesema uuzwaji wa gari hizo umewekewa urahisi kwani mtu ataweza kulipa kwa kila mwezi “Tunafikiria kujenga kiwanda cha kuunganishia magari hapa kwa baadaye ili kuendelea kuweka unafuu zaidi wa bei ya magari yetu”.
Mkuu wa Tata Holdings Limited kanda ya Arika Mashariki, amrsema: “Hii ni hatua ya kwanza kubwa kufikiwa . Tunajivunia na tuna imani kuwa tutafanya hivi tena katika bidhaa nyingine bora kwa siku zijazo.”
Pichani juu na chini ni aina ya Magari ya Tata HEXON na Tata HEXA yamezinduliwa na Kampuni ya Magari ya TATA Motors kwa kushirikiana na msambazaji wake nchini Tanzania Tata Africa Holdings
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...