*Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019 badala ya Julai
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.
Amesema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi Soga, Pwani.
“Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii.”Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.
Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”
Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.Alisema mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni 2.7.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli
ya SGR wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Markezi inayojenga
Reli hiyo, katika eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam, Novemba 3,
3018

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya ujenzi wa madaraja ya
kupitisha treni juu wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi
Merkezi inayojenga reli ya Kisasa ya SGR Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo
ipo eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya
SGR wakati alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo
la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani,
Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa reli ya SGR katika eneo
la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...