Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akimkabidhi majarida na vipeperushi vya utalii wa Tanzania (promotional materials) Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara, Andrew Rosindell .

Na Geofrey Tengeneza

Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara Mheshimiwa Andrew Rosindell ameahidi kusaidia kufanikisha mpango wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kufanya Safari zake London, Uingereza.

Mheshimiwa Rosindelli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na kuwa na mzungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa WIzara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki katika maonesho ya utalii ya World Travel Market yanayoendelea jijini London Uingereza ambapo alimuomba mwakilishi huyo kusaidia mpango huo ambao alisema utasaidia sana kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania kutoka Uingereza.

Aidha Dkt.Nzuki amemuomba Mheshimiwa Rosindell kuandaa mkutano wa pamoja baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza mapema iwezekanavyo ili kujadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Aidha, Dkt.Nzuki ameweza kukutana na kufanya mazungunzo na Mjumbe maalum ambaye pia ni Mbunge wa nchi hiyo Andrew Rosindell ambaye ni mbunge aliteuliwa na Waziri Mkuu huyo kuwa Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza wa masuala ya Biashara (Trade Envoy) ambaye miongoni mwa kazi zake ni kukuza biashara, uwekezaji na Utalii baina ya Uingereza na Tanzania.
Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara, Andrew Rosindell akisoma moja ya majarida ya utalii alipotembelea banda la Tanzannia katika maonesho ya World Travel Market jijini London Uingereza.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla amepongeza timu ya Tanzania inayoshiriki maonyesho hayo kwa kazi nzuri ya kuitangaza vyema Tanzania kama eneo bora la utalii Afrika na Duniani kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake Twitter aliandika "hii ni taswira ya leo ya banda letu la maonesho kule jijini London, kwenye World Travel Market (WTM), Uingereza, ambapo slogan yetu ya Tanzania: Unforgettable! imetumika ipasavyo kuuza vivutio vyetu. Nawapongeza sana washiriki wote kutoka Tanzania na wa Kamati yetu ya Destination Branding chini ya uenyekiti wa Ndg. Devotha Mdachi kwa kazi nzuri. Huu ni mwanzo tu” aliandika DKt Kingwangala.

Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umeratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania –TTB ambapo timu ya washiriki kutoka Tanzania ikijumuisha waoneshaji kutoka sekta ya umma na binafsi inaongozwa inaongozwa na Naibu Katibu MKuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...