Na Mwandishi wetu,
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limewataka walimu nchini kuendeleza juhudi wanazozionyesha katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili kuendelea kuinua kiwango cha elimu kinachotolewa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Elimu kutoka UNESCO, Faith Shayo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali kwa walimu na wadau iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha ‘America Corner’ uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutambua michango mbalimbali ya walimu hao katika ufundishaji na maeneo mengine ambayo kimsingi yanaleta tija katika kukuza maendeleo ya Taifa.
Alisema licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, walimu nchini wamekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao, suala alilowataka kutokufa moyo na badala yake kuongeza bidii.
“Sote tunashuhudia namna ambavyo walimu wanavyojitahidi kutimiza wajibu hao kikamilifu kila siku licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu katika kuinua maendeleo ya Taifa” alisema Faith.
Alisema tuzo hizo zinapaswa kuchukuliwa kama changamoto na walimu hao kwa kufanya vizuri wakati wote wanapotimiza wajibu wao wa kazi, hatua ambayo pamoja na sababu mengine zitawafanya wazidi kupata mafanikio.
Aidha alimpongeza muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda kwa kubuni wazo hilo lililolenga kutambua mchango wa walimu nchini, suala alilosema kuwa kwa kiasi kikubwa litazidi kuwapa moyo wa kazi walimu hao.
Awali muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda, alisema ‘How is My Teacher’ ni wazo alilolibuni kwa ajili ya kutambua mchango unaotolewa na walimu wote hapa nchini ikiwa na lengo la kuwahamasisha kuongeza msukumo katika utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji.
Alisema tuzo hizo ambazo ni mara ya kwanza mwaka huu, zinatarajiwa kuwa endelevu kila mwaka kwa lengo la kuendeleza utamaduni wa kutambua mchango wa walimu hao.
Jumla ya tuzo kumi zilitolewa kwa walimu mbalimbali waliopatikana kupitia mchakato maalumu wa uliowahusisha wanafunzi kupendekeza walimu wao na baadae kupigiwa kura.
Mgeni
rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akizungumza na
walimu pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati hafla ya utoaji
tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu
iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America
Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi
wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda akizungumzia
mchakato uliopitiwa mpaka kuwapa washindi wakati hafla ya utoaji tuzo na
kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na
‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo
la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwalimu
wa Shule ya Sekondari Msimbazi ambaye pia ni Mwalimu wa Elimu maalum wa
shule ya walemavu Kimanga Sekondari , Bi. Sylvia Ruambo akielezea
furaha yake baada ya kupokea tuzo wakati hafla ya utoaji tuzo na
kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na
‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo
la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi tuzo
mshindi wa kategori ya mtu aliyefanya vyema katika utoaji wa huduma za
elimu, Bi. Sylvia Ruambo (katikati) wakati hafla ya kutambua michango
inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na
kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya
Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni
Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda
Mkuu
wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akimkabidhi tuzo mshindi wa
kategori ya mtu aliyewezesha changamoto kuondolewa katika utoaji wa
huduma za elimu kutoka Visiwani Zanzibar, Bw. Ami Vuai (katikati) wakati
hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini
iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America
Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT
Awards), Bw. Raymond Luanda
Mgeni
rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto)
akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu wa mfano katika utoaji wa
huduma za elimu nchini, Bw. John Bosco (katikati) wakati hafla ya
kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini
iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America
Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT
Awards), Bw. Raymond Luanda.
Mgeni
rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika
picha ya pamoja na baadhi ya walimu walioshinda tuzo pamoja na
wawakilishi wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma
za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye
ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa
jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...