NA MWAMVUA MWINYI, PWANI .

JUMUIYA ya wanawake ya Chama Cha Mapinduzi (UWT) mkoani Pwani, imempa big up ,Rais Dk. John Magufuli kwa kasi yake ya utekelezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo miradi ya REA awamu ya III kwa vijiji 150 na mradi mkubwa wa Rufiji Hydropower utakaozalisha 2,100MW baada ya kukamilika .

Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga bajeti ya bilioni 12.4 kwa ujenzi wa vituo 18 vya afya mkoa mzima na hospital tatu Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti. 

Awali akiishukuru serikali Mbunge wa viti maalum mkoani hapo, Subira Mgalu, wakati wakisheherekea miaka mitatu ya Rais Magufuli akiwa madarakani, sherehe iliyodhuriwa pia na kamati ya utekelezaji ya UWT mkoa. Anasema"Nikianzia sekta nayoisimamia nikiwa naibu waziri wa nishati nampongeza kupitia uongozi wake na maelekezo yake kuwasilisha bajeti ndani ya bunge ,wizara ya nishati imekuwa ikipata ongezeko kila mwaka "

"Wakati akiingia madarakani mh Rais alikuta asilimia 38 ya wanapata huduma za umeme lakini sasa ni asilimia 60 wamepata umeme kupitia miradi iliyokaribu nao, na miradi ya umeme vijijini "alifafanua Subira. Subira alielezea, kuna REA awamu ya tatu ambayo inaendelea ambapo vijiji 7,873 vilikuwa havina umeme lakini kwa kazi inayoendelea mzunguko wa kwanza vijiji 3,559 vinafanyiwa kazi na wakandarasi wapo kazini .

Alibainisha kwamba, kulikuwa na mradi wa ujazilizi ambapo vijiji 105 vimepata umeme na wananchi zaidi ya 25,000 kwenye mikoa nane ukiwemo nane wameunganishiwa umeme na mradi unaendelea .Hata hivyo alisema, serikali hiyo imeweza kufanikisha miradi ya maji katika miji ya Bagamoyo, Kibiti ,Utete pamoja na mradi wa maji WAMI -Chalinze ,Ruvu -Chalinze -Msoga, mradi wa maji katika miji ya Kisarawe na Mkuranga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...