Wajasiriamali Nchini kuendelea kunufaika na Mpango wa Kurasimisha Biashara katika mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaniunua wajasiriamali hao.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe yanayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kuongeza tija na kuchangia katika ujenzi wa Taifa, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao.
“Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Bunge kwa kuiwezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi hasa katika eneo la kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili warasimishe Biashara zao;’’ Alisisitiza Mgembe
Akifafanua amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo Wajasiriamali hao yameendeshwa kwa siku 10 ambapo kila kundi lilikuwa na siku mbili za kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo benki kama; CRDB Bank na NMB .
Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kutoa mada katika mafunzo hayo ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na wataalamu wengine wa ujasiriamali.
Pia, alipongeza ushirikiano ulipo kati ya MKURABITA na Mkoa wa Njombe hali iliyosaidia katika kufanisha mafunzo kwa wajasiriamali na pia urasimishaji ardhi kwa wananchi ambapo baadhi yao wameweza kupata mikopo katika Taasisi za fedha na hivyo kuinua uchumi wao kutokana na kukua kwa shughuli za ujasiriamali walizokuwa wanafanya na hasa kutokana na mikopo waliyopata kutoka katika Taasisi za fedha zikiwemo Benki. 

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania
(MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe
akizungumza na sehemu ya wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji wa Njombe wakati
wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biasharaza zao hali
itakayowawezesha kuongeza tija na kupata mikopo katika Taasisi za fedha.hiyo
ilikuwa Novemba 16,2018 Mkoani Njombe.
Sehemu
ya Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe wakimsikiliza Mratibu wa Mpango
wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi.
Seraphia Mghembe (Hayupo pichani) leo mjini Njombe wakati wa mafunzo kwa
wajasiriamali wa Halmashauri hiyo
yanayolenga kuwajengea uwezo wa kurasimisha Biashara zao.
Afisa
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa
wa Njombe Bw. Stanley Sulle Akiwasilisha mada kwa wajasiriamali hao kuhusu
taratibu za ulipaji kodi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze
kurasimishaji biashara zao na hivyo kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kulipa
kodi, Mafunzo hayo yameandaliwa na MKURABITA.
Mmoja
wa wajasiriamali waliopata mafunzo ya
kujengewa uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bi. Sesilia Mwalyego akizungumza
katika mafunzo hayo leo Mjini Njombe, Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya
Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao.
Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na urasimishaji wa Ardhi Bw. Bahati Mtitu akionesha jinsi alivyoiweza kupanua na kukuza shughuli zake za ujasiriamali baada kurasimisha ardhi na kupata hati zilizomuwezesha kukopa katika Taasisi za fedha
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...