WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametembelea kituo cha afya cha Nkowe na kuwataka wananchi wakilinde na kukienzi kwa kuwa ndio mkombozi wao kiafya.Amesema kwa sasa wananchi hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ametembelea kituo hicho cha afya leo (Jumapili, Novemba 18, 2018) akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.Ametaja baadhi ya huduma zinazopatikana kwa sasa kwenye kituo cha Afya Nkowe ambazo awali hazikuwepo kuwa ni pamoja na upasuaji, maabara, mama na mtoto.“Rais Dkt. John Magufuli anataka kila Mtanzania apate huduma za afya karibu na makazi yake ili asilipe nauli au kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.”

Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na huduma zinazotolewa kituoni hapo, ambapo amewataka watumishi waendelee kuwahudumia wananchi vizuri.Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho cha afya wameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini, ambapo kwa sasa wanatibiwa karibu na makazi yao. Awali, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Paul Mbinga alisema kituo hiko kinahudumia jumla ya wakazi 5,264 wa kata ya Nkowe pamoja na wananchi wa kata za jirani za Chienjele, Nandagala, Likunja na Mnacho. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa na Bibi Asia Abdallh (kushoto) wakati alipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo hicho Novemba 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo wa utakatishaji vifaa vya  upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Novemba 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi khanga Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Grace Nanguka ikiwa ni zawadi ya watumishi wote wa Kituo hicho wakati alipokagua ujenzi na ukarabati wa Kituo hicho, Novemba 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Walimu na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za wilaya ya Ruangwa kwenye ukumbi wa Narung’ombe, Novemba 18, 2018. Kulia ni Mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...