Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia) akitizama mboga
za majani zilizokaushwa na kuhifadhiwa katika paketi kwa ajili ya
kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka kikundi cha Amka
Group cha Tabora Mjini kushoto ni Mjasiriamali wa kikundi hicho Bi.Anna
Shango ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na
Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora (wapili kulia) ni Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda uwanja wa Jeshi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akitizama viungo vya
mbalimbali vya chakula vilivyosagwa na kuhifadhiwa katika vikopo kwa
ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Wilaya
ya Uyui ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na
Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kushoto) na Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (katikati) pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri wakifurahia maziwa
yanayotengenezwa na Neema Brand mjasiriamali mdogo wa Mkoa huo leo
walipotembelea Maonesho ya wajasiriamali waliyoshiriki maonesho ya
Jukwaa la Fursa za Biashara katika uwanja wa Jeshi linaloendelea Mkoani
hapo,kushoto ni Bi.Sameera Sumar mmilikiwa biashara hiyo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitizama zulia
lillofumwa kwa mikono na Mjasiriamali Bw.Hassan Rashid (kulia) kwa
kutumia mikono na mifuko ya sandarusi iliyokwisha kutumika na nzuri
leo alipotembelea maonesho ya wajasiriamali waliyoshiriki Jukwaa la
Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora katika
uwanja wa Jeshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...