Meli Mpya ya Kampuni ya Usafiri wa Baharini ya Sea Star  yenye uwezo wa kubeba Mizigo Tani 1,400 na Abiria 1,500  imewasili Bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuongeza huduma za Usafiri wa Baharini katika Mwambao wa Bahari ya Afrika Mashariki. Meli hiyo iliyopewa jina la Sea Star 1 itafuatiwa na Boti nyengine Mbili za Mwendo wa Kasi zinazotarajiwa kuingia Visiwani Zanzibar Mwezi Juni Mwaka ujao wa 2019.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mamlaka zinazosimmamia Usafiri wa Baharini alipata nafasi ya kukagua sehemu mbali mbali za Meli hiyo iliyopo Bandaini Malindi na kuridhika na Ubora wake. Meli hiyo yenye sehemu kubwa ya kubebea Mizigo, Vyumba vya Watu Mashuhuri { VIP} pamoja na Abiria wa kawaida itaanza na safari za Zanzibar-Pemba – Tanga, Zanzibar – Dar es salaa, Zanzibar – Mtwara na baadae kuendelea na safari za mbali kwa kuanzia Visiwa vya Comoro.


Safari ya Zanzibar - Dar es salaam huchukuwa muda unaokadiriwa wastan wa saa Tatu wakati safari ya Zanzibar – Pemba itachukuwa wastani wa saa Nne na Nusu. Akitoa Maelezo ya uwepo wa Meli hiyo Nchini Mwakilishi wa Kampuni ya Sea Star Mh. Salum Turky alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umejizatiti kutoa huduma bora za Usafiri wa Baharini kwa Wananchi wote.

Kepteni wa Meli Mpya ya Sea Star Nassor Abubakar akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Chumba cha Mawasiliano alipofika kuikagua Meli hiyo.
Balozi Seif na mwenyeji wake Mh. Salum Turky wakipumzika moja ya sehemu za VIP baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Sea Star Mh. Salum Turky wa Tatu kutoka Kulia akisisitiza azma ya Uongozi wa Kampuni hiyo kufuata Taratibu zote za usafiri wa Baharini wakatiu choba chao kitakapoanza kutoa huduma ya usafiri.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Uongozi mzima wa Sea Star juu kabisa ya Meli ya Kampuni hiyo baada ya kumaliza ziara ya kuikagua sehemu mbali mbali. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...