Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BARAZA la Sanaa la Taifa ( BASATA) limewaruhusu wasanii Nasib Abdul 'Diamond Platnumz' na Raymond Mwakyusa 'Rayvan' kufanya maonesho nje ya nchi.

Wakitoa taarifa hiyo leo, BASATA wamesema kuwa wasanii hao walikuwa wameshaingia mikataba inayofahamika katika nchi mbili za jirani kabla ya adhabu ya BASATA kutolewa.

Wamesema kuwa, kwa kuzingatia mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na nchi nyingine lakini pia kwa upande wa mashabiki tayari walikuwa wameshakata tiketi za maonesho hayo.

Kupitia taarifa hiyo BASATA limewaondolea katazo la maonesho hayo tajwa tu na kubakiza katazo la ndani ya nchi mpaka pale Diamond na wenzake watakapoonesha mabadiliko chanya kitabia.

Mbali na hiyo, BASATA limeonekana kutokuridhishwa na baadhi ya waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuuim ana kucheza wimbo huo kwa bashasha na nderemo ukiwa tayari umeshafungiwa bila kujali athari zake kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

BASATA wanawasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nyimbo zote zilizofungiwa haziruhusiwi kwa namna yoyote kutumiwa na jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...