Na Abdullatif  Yunus wa Globu ya Jamii, Kagera
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt Bashiru Ally Kakurwa amewasisitiza wale wote wanaohitaji Uongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, Kujipanga kwa Sifa, Sera nzuri zitakazowauza na si kwa kurubuni, wala kuhonga Wananchi.
DKT. Bashiru amesema hayo Desemba 22, 2018 Baada ya kuwasili Nyumbani kwao Kanazi Mkoani Kagera wakati akizungumza na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Wananchi Waliojitokeza Kumpokea na Waliomsindikiza hadi Nyumbani kwake Nje kidogo ya Mji wa Bukoba.
Dkt. Bashiru amesisitiza juu ya Wagombea kufanya Siasa za Maendeleo, na sio Siasa chafu za Kugawa watu, kujikomba, kurubuni wala kutoa hongo huku akiwataka Wanachama Kuanza kubaini Wanachama wenye sifa, wenye Uchu na Maendeleo  na wasioweka weka mbele masilahi yao Binafsi, ili Uchaguzi ujao uwe wa Mfano, kama Chaguzi Zilizofanyika enzi za TANU.
Sambamba na hilo Dkt. Bashiru amenukuliwa akisema kuwa Kiongozi atakaechaguliwa kwa kutumia Njia za Ulaghai hata kama atakuwa amepitishwa, akibainika ataenguliwa mara moja.
Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amewataka Viongozi waliopo Madarakani waachwe wafanye Kazi, Kwani Muda wa Kuanza kunadi Sera bado, hivyo kwa wale ambao wameaanza kupita pita kwa Wanachama waache Mara moja kwani tayari Orodha yao tayari anayo kwa Nchi nzima. 
 Kuhusu wawekezaji, Dkt. Bashiru amesema Nchi ya Tanzania Bado ni maskini na Nyenzo pekee ya kujikwamua kutoka katika Umasikini huo ni kupitia Sekta ya Kilimo, hivyo hapendezwi na hali iliyopo kwa sasa ya kuwaruhusu wawekezaji kutoka Nje ya Nchi kufanya shughuli za Kilimo, Ufugaji Na Uvuvi hapa Nchini. Hivyo amemuagiza Naibu Waziri wa Kilimo Ndg. Innocenti Bashungwa kuwa kwa wale ambao wameshapewa nafasi ya Kufanya shughuli hizo wawe wa mwisho,  na kwamba Ardhi ya Tanzania ilimwe na Watanzania wenyewe, na kuanzia sasa Wizara haitatakiwa kutoa Vibali kwa wawekezaji katika Sekta ya Kilimo kufanya Kilimo ndani ya Nchi yetu.
Dkt. Bashiru yupo Mkoani Kagera kwa Mapumziko mafupi pamoja na Ziara ya Kikazi Ambapo Kuanzia Desemba 26, Mwaka huu ataanza Ziara hiyo kwa kukutana na Viongozi wa Chama Kutoka Missenyi, Bukoba na Bukoba Mjini.
Mzee Masabala Akiongoza tukio la Kumsimika Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Kuwa Chifu mara baada ya Kuwasili Kijijini Kwao Kanazi - Bukoba.


 Dkt. Bashiru Anaonekana ameshikilia  Mkuki na Mundu Mara Baada ya kusimikwa na Wazee wa Kimila.
Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu CCM - Taifa Akizungumza na Wananchi pamoja na Viongozi wa Serilkali na Chama, Nyumbani Kwao Kanazi, Kemondo mara Baada ya ulakiwa na Kusimikwa na Wazee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...