Mishahara ya Waajiri na Maafisa Utumishi watakaobainika kuwasilisha taarifa za kiutumishi zisizo sahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS) itasimamishwa mara moja na Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuwakumbusha waajiri na maafisa hao kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi na kwa wakati.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kufahamu vema majukumu ya idara hiyo.

Ili kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kutosita hata mara moja kusimamisha mshahara wa mwajiri au afisa utumishi yeyote atakaebainika kuwasilisha taarifa zenye udanganyifu na kuwataka kutozifanyia kazi na kuzirejesha mara moja kwa waajiri na maafisa hao.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameainisha kuwa, lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa Ofisi ya Rais-Utumishi hata kosa linapokuwa kwa waajiri, hivyo amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatenda haki kwa kuwasilisha taarifa sahihi na kwa wakati ili ziweze kufanyiwa kazi.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya  Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimali Watu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Ibrahim Mahumi (kushoto) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...