Na Abdullatif  Yunus wa Globu ya Jamii, Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ameanzisha kampeni hiyo ya kutokomeza Udumavu wa watoto Mkoani Kagera, Desemba 26 wakati wa  ukaguzi wa kiwanda cha kuchakata Nyanya  ili kupata "Tomato sauce" Kiitwacho VICTOLIA EDIBLES LTD    Kilichopo eneo la Kafunjo Kata Butelankuzi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.


Akiwa katika ukaguzi huo katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally amewaaka viongozi wote  wa Chama  na serikali kuendeleza kampeni hii ili kupunguza udumavu wa watoto Mkoa wa Kagera "Kagera ni Mkoa wenye  vyakula vingi vya asili na ardhi yenye rutuba ya kustawisha mazao mengi kama Ndizi ,Mahindi, Mihogo hivyo haipaswi kuwa na ongezeko kubwa la watoto wadumavu "amesema Katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally Mkuu 



Aidha amewasisitiza viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kuelimisha Watanzania namna yakupata lishe bora ili kutokomeza Udumavu wa watoto hasa Mkoa wa Kagera.

Ziara hiyo fupi ya Katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally ameongozana na Mbunge wa CCM  Bukoba Vijijini na Katibu wa wabunge wa Chama hicho  Mh.Jasson Rweikiza (MB), Ziara hiyo imesababisha Katibu kuzuru eneo la Kanazi na  kukagua eneo ambapo kitajengwa Kituo cha Afya ya Wilaya ya Bukoba.

Akizungumza mbele ya wananchi amewataka Wanakagera  na Watanzania wote kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli kwa juhudi anazozifanya za kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati na kuendeleza kampeni ya Tanzania ya Viwanda

 Mh.Jasson Rweikiza (MB), Mkurugenzi wa Kiwanda cha Victoria Edibles Ltd akitoa maelezo ya mitambo, pembeni ni Mh. Dk. Bashiru Ally Katibu wa CCM - Taifa
 Sehemu ya kiwanda Cha kuchakata Nyanya Victoria Edibles ltd kilichopo Kafunjo Bukoba, Kagera.
Mh. Bashiru, na Mh. Rweikiza wakikagua eneo ambapo Hospitali ya Wilaya ya Bukoba inatarajiwa Kujengwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...