Wilaya ya Kigamboni imeongoza katika utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali katika mpango wa kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuwa ya kwanza katika Mkoa wa Dar es salaam kuwafikia wafanybiashara wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri alipokutana na wandishi wa habari ofisini kwake  jana. Mkuu wa Wilaya amesema ofisi yake ilipokea vitambulisho elfu tano toka ofisi ya Rais-Tamisemi na vikiwa na lengo la kukusanya jumla ya shilingi Milioni mia moja lakini mpaka jana Desemba 28,2018 jumla ya shilingi milioni 94 sawa na asilimia 97 ya lengo.

  Mkuu wa Wilaya amesema  kuwa kiwango hicho kimefikiwa baada ya kuwa na mpango wa ushirikishwaji wa watendaji wa mitaa na wenyeviti ambapo waliweza kuwafikia wajasiriamali wengi katika mitaa yao.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Temeke Bw.Gamaliel Mafie amesema wao kama mamlaka wamefurahia huo mpango kwa kuwa umewajumuisha watu ambao hawakuwa kwenye mfumo rasmi wa walipa kodi. Ameongeza kuwa hata wao wamepokea mpango huo kwa furaha kwa kuwa umepanua wigo wa walipa kodi kwa mpango wa kuchangia.

Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Wilaya  ametuma ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili aweze kupatiwa vitambulisho elfu tatu (3000), kukidhi idadi kubwa ya wafanyabishara ambao bado hawajafikiwa mpaka sasa.
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akimkabidhi kitambulisho cha mjasiriamali,Amina Rashidi jana  jijini Dar es Slaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Temeke,Gamaliel Mafie akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika jana  jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...