NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

JESHI la polisi mkoani Pwani, kupitia kikosi cha usalama barabarani limekusanya kiasi cha sh. milioni 228.440 za madeni ya makosa ya usalama barabarani .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema ,fedha hiyo imepatikana kutokana na madereva waliofanya makosa kipindi cha nyuma kutakiwa kufanya hivyo . 

Alieleza, kwa muda mrefu kumekuwepo na tabia kwa madereva wanaofanya makosa na kuandikiwa kulipa tozo la serikali kwa njia ya POSS mashine kushindwa kufanya hivyo kwa dhana ya kuwa hawataweza kubainika kwa kuwa mfumo mpya wa ulipaji wa tozo humtaka dereva husika kwenda kulipia yeye ndani ya siku saba. 

Wankyo aliwataka, madereva ambao wanatambua kuwa wanadaiwa kulipa mara moja kwani hatutakuwa na muhali nao pindi watakapowakamata.Kamanda huyo alifafanua ,wanaendelea kupambama na mabasi yanayosafiri kupitia barabara za mkoa wa Pwani kwa kuyakagua na kuona kama yana ubora wa kufanya usafirishaji wa abiria. "Kudhibiti ujazaji ndani ya mabasi kwa kuweka abiria kwenye vigodoro, uzidishaji wa nauli kwa abiria kwa kushirikiana na SUMATRA, malori na kuyafanyia ukaguzi wa kina katika maeneo yao ya maegesho na yanapopita kwenye barabara zetu "alisisitiza. 

Wankyo alisema ,watadhibiti usafiri wa magari madogo aina ya Noah yanayobeba abiria kwa kushirikiana na SUMATRA yasizidishe abiria na yasiende umbali wa kilometa zaidi ya 50#.Pamoja na hayo wana mikakati waliyojiwekea kuendelea pia kutoa elimu kwa madereva wa pikipiki katika wilaya zote wapatao 444.

Alielezea, lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanapunguza ajali kwa waendesha pikipiki ambao wengi wao wamekuwa hawakidhi vigezo vya kuendesha vyombo vya moto, kutojua sheria na kanuni za usalama barabarani na udereva wa kujihami.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...