*Ni kupitia kauli mbiu yake ya Jitambue,mabadilika,acha mazoea...Makonda atoa neno


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MASHEIKH wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( BAKWATA) katika mikoa yote ya Tanzania wamempongeza Sheikh Mkuu Aboubakary Zubeiry kutokanana namna ambavyo amejenga umoja na mshikamano ndani ya baraza hilo.

Wametoa kauli hiyo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 ya BAKWATA tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968.Akizungumza kwa niaba ya masheikh wa mikoa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema wanampongeza wanampongeza Muft Zubeiry kwa namna ambavyo amefanya mabadiliko makubwa ya kuwaunganisha Waislamu nchini.

"Wakati leo tunasheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa BAKWATA ,salamu za kipekee tunazipeleka kwa Mufti wa Tanzania kwani maadhimisho hayo yanamkuta yakiwa mikononi mwake."Chini ya Mufti wetu Sheikh Zubeiry BAKWATA imekuwa mpya,na walio chini yake tunapendana,tunaheshimiana na tunajitambua .Kupitia kauli mbiu yake ya Jitambue, Mabadilaka,Acha mazoea hakika imetusaidia kutubadilisha na kila mmoja wetu anajua majukumu yake," amesema Sheikh Alhad.

Amesisitiza kupitia Mufti wa Tanzania BAKWATA imeunganishwa na walio chini yake wamekuwa waaminifu na walio tayari kuhakikisha baraza hilo linasonga mbele kimaendeleo.Pia amesema kuwa BAKWATA kwa sasa wamekuwa na uhusiano mzuri na taasisi nyingine na chini ya Mufti Zubeiry kuna maendeleo makubwa yanaendelea kufanyika ukiwamo wa ujenzi wa msikiti mkubwa ambao unajengwa katika makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...