MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti
wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, kwa ajili ya
Michuano ya Vijana Mpira wa Miguu Jimbo la Tunguu, vilivyotolewa na
Mbunge na Mwakilishi. kushoto Katibu wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Ndg.
Ali Khatib Kisu, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga
Bweni.(Picha na Othman Maulid)
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akipata maelezo ya Bidhaa
zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Maendeleo cha Vijana Ubago Bi.
Hawa Ali Mzee, akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana
hao, akiangali Shampoo wakati akitembelea kikundi hicho,kushoto
Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg.Said Hassan.(Picha na Othman
Maulid)
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, akiangalia Shampoo inayotengenezwa na
KIkundi cha Vijana cha Maendeleo Ubago, akipata maelezo kutoka kwa
Katibu Hamasa wa Kikundi hicho Bi. Hawa Ali Mzee, wakati alipotembelea
kikundi hicho Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Othman Maulid)
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiangalia moja ya nguo zinazozonwa
na Kikundi cha Vijana na Maendeleo Ubago, wakati alipowatembelea Vijana
hao katika Kituo chao kuangalia shughuli wanazozifanya za utengenezaji
wa Shampoo, Sabuni. Lotion na mafuta ya mgando na ushoni wa nguo.(Picha
na Othman Maulid)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...