*Ameagiza ifikapo January 2019 hataki kuona matatizo hayo, ataka wajirekebishe.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe amelalamikia huduma zinazotolewa kwa Wateja na Kampuni ya Ndege (ATCL) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.

Akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya, Mhandisi Kamwelwe amesema huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo zimekuwa zikilalamikiwa na Abiria ambapo ametolea mfano uwepo wa Joto kali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Terminal 2).

Ameagiza kuwaondolea usumbufu Abiria wanaosafiri ambapo amesema abiria hao lazima wasikilizwe uhitaji wao.Pia ametaka kuendeleza ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Songwe kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa Kiwanja hicho kinachotegemewa kutua Ndege mpya. Pia kuhusu sakata la Fastjet, Mhandishi Kamwele amesema kuwa Kampuni hiyo tayari ilipewa agizo la kujirekebisha hivyo walipewa siku 28 ambapo zikiisha imeelezwa hatowezo kufanya biashara hapa nchini, na hatoweza kufanya biashara sehemu nyingine mpaka alipe madeni ya Serikali.

Ameagiza Rubani wote na Watendaji wa SUMATRA kutokwenda likizo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuhakikisha uhitaji bora wa usafiri kwa abiria. Amesema hakuna atakayeongeza bei ya nauli katika usafiri.Amesema Ndege za AirBus za ATCL kuwasili Desemba 23, 2018 kama ratiba haijabadilika ambapo amesema tayari imetuma Crew wakiwemo Rubani nchini Canada kwa mafunzo. Uwanja wa Ndege Terminal 3 kukamilika mwezi May mwakani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Richard Mayongela amemuahidi Waziri Kamwele kushughulikia changamoto zote ambazo zimelalamikiwa kwa Mamlaka hiyo katika utoaji huduma ifikapo January Mosi, 2019 ka ilivyoagizwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandishi Isack Kamwelwe akizungumza na Mejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini baada yakurejea kutoka kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Richard Mayongela akitoa ufafuzi kwenye kikao cha pamoja baina ya Menejimenti ya Mamlaka hiyo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo ameahidi kutatua changamoto ambazo zimetajwa katika Mamlaka hiyo.

Sehemu ya Menejimenti ikimsikiliza Waziri alipokuwa anazungumza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...