GOLI LA CHAMA SHANGWE KAMA ZOTE MSIMBAZI...ROHO KWATUU
*Injiniaaa soma ngapiiiii hiyo ? Simba 3 ,Nkana 1...Simba yaingia hatua ya makundi kwa kishindo
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
Simba...Simba...Simba...Eee kidedea ...pipipipii eee kidea!Hivyo ndivyo ilivyokuwa inasikika ndani ya Uwanja Mkuu was Taifa jijini Dar es Salaam.
Unajua kwanini? Ngoja nikusimulie hiyo ilitokana na Bao l Tatu la Simba SC lililofungwa na Kiungo Maestro, Clautos Chotta Chama 'Mwamba wa Lusaka' ambalo lilitosha kuipeleka timu hiyo hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa mashabiki wa soko ,wakereketwa na wachama wa Simba walijikuta wakiwa na furaha iliyopitiliza kiasi cha hakuna aliyeweza kujizuia kuionesha .Kila aliyekuwepo uwanjani ulikuwa ni kwendo was shangwe.
Moja ya swali kubwa ambalo lilikuwa linaulizwa na mashabiki was Simba ni je kuna mtu anayeseka ? Na kama yupo anyooshe mkono afanye kama anajikuna.Baadhi ya mashabiki was Simba ambao wamezungumza na Michuzi Blog baada ya kumalizika kwa mpira huo wamekiri kufurahishwa na matokeo ya timu yao ambayo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Wamesema haikuwa kazi nyepesi kuifunga Nkana ambayo imeonesha uwezo wa kumiliki soka la hali ya juu ambayo iliifanya wachezaji wao kupotea kwa nyakati tofauti tofauti na hasa kipindi cha pili."Simba leo imenifurahisha ,imetufanya tutembee kifua mbele maana upande wa pili walikuwa wanatuombea tufungwe.Leo wanateseka kwa matokeo ambayo tumeyapata.
"Mechi hii kwetu ilikuwa ni kufa au kupona na hatimaye tumepona," amesema mmoja was shabiki wa Simba aliyejitambulisha kwa jina moja la Jumanne mkazi Dar es Salaam.Kwa kukumbusha Nkana walikuwa wa kwanza kupata goli na kuifanya Simba kupoteza furaha kwa muda hadi pale mchezaji wake Jonasi Mkude alipoipatia bao la kusawazisha kabla ya Medie Kagere kufunga bao la pili dakika chache kabla ya mapuziko.
Mchezo wa Simba kwa siku ya Jana wenye macho wameona na wenye masikio wamesikia,hata hivyo kubwa kwa Simba wameweka rekodi ya kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ambapo kwa mara ya mwisho waliingia hatua hiyo mwaka 2003.
Hata hivyo nje ya uwanja shangwe zilikuwa kama zote na moja ya shabiki yeye alikuwa anauliza hivi "Injinia somaa ngapi hiyooo? Majibu ya mashabiki wenzake wa Simba yakawa ni Simba tatu na Nkana moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...