Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam Bi Jane Jisandu, ameibuka mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo.

Jane anakuwa mshindi wa tano wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaam, Mbwana Mbela mkazi wa wMpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam, Jane alisema zawadi hiyo ni muujiza na kuongeza kuwa itasaidia kuokoa maisha ya mwanaye ambaye anatakiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu.“Kwangu huu ni muujiza mkubwa sana. Nina mtoto mgonjwa na ambaye nimeambiwa anaweza kutibiwa lakini mpaka nchini India. Gharama za matibabu yake ni kubwa, nilikuwa nikiwaza wapi ningepata fedha za matibabu lakini Mungu amenitendea muujiza kupitia Tigo, naishukuru Tigo kwa kuokoa maisha ya mwanangu,” alisema

Jane alisema amefanikiwa kushinda zawadi hiyo baada ya kuwa antumia huduma za Tigo kama kuweka kuma wa maongezi, kununua vifurushi mbali mbali pamoja na kutuma pesa kwa njia ya Tigo Pesa huku akiwataka watu kutumia huduma za Tigo ili kujishidia zawadi za fedha taslimu.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa pili kushoto) akifurahia mfano wa hundi  kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa (wa pili kulia). Wanaoshguhudia wa kwanza kushoto ni mtangazaji wa radio clouds FM Mina Ally na wa kwanza kulia ni Deogratius  David kutoka Tigo.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa tatu  kushoto) akiwa kaika picha ya pamoja na washindi wa shilingi milioni moja moja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...