Na WAMJW – MISUNGWI, MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kuhakikisha wanakamilisha kuleta vifaa vyote vinavyohitajika katika vituo vya Afya vinavyoboreshwa nchini kabla ya Januari 15, 2019 ili wananchi waweze kupata huduma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy wakati akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije na kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

“Haina maana ya kuwa na majengo makubwa na mazuri ya Vituo vya Afya kama hakuna vifaa vinavyohitajika, huku Wananchi wanaendelea kupata tabu”, alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewahasa Wazazi na Wananchi wote kwa ujumla kutodharau huduma za Chanjo, hivyo kuwahimiza Wananchi wote kuwapeleka katika vituo vyakutolea chanjo watoto waliofika umri wa kupata chanjo

“Kifafa, Kifaduro,Donda koo, Surua, hayapo siku hizi kwasababu ya Chanjo, kwahiyo tusije tukadharau chanjo, tuhakikishe kila mtoto mwenye umri wakupata chanjo , akapate chanjo” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifunua kitambaa, ishara ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije, ikiwa in sehemu ya majukumu katika ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiendelea na ukaguzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Koromije, ikiwa in mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. 
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe.Charles Kitwanga akisema jambo mbele ya wapiga kura wake (hawapo kwenye picha) katika kijiji cha Koromije Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Waziri wa Afya ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya kijijini hapo. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihutubia wanakijiji wa Koromije (hawapo kwenye picha) pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. . 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia gharama za matibabu kwenye mbao ya matangazo katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...