Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, mapema leo amekutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mbali na maagizo na maelekezo mbalimbali aliyowapa, lakini pia aliwachangia fedha taslim shilingi Laki Tano ( 500,000/-)  ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM ambapo inahitajika milion 2 kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.

Ndg Kadege amesisitiza hadi januari mwishoni lazima tuwe tumemalizana na jambo la fidia kisha tuanze mchakato mapema wa kupata hati na kuanza kutekeleza mipango yetu ya kuhakikisha UVCCM tunakuwa na miradi mbalimbali  na kukuza uchumi na kujitegemea ili kuepukana na hii omba omba toka kwa wadau ambao mara zote wamekuwa na masharti ya kiuchaguzi.

Pia kamati ya Utekelezaji UVCCM wilaya ya Ileje ilimpatia zawadi ya kuku kwa ajili ya Christmass.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje  ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM, ambapo inahitajika milion mbili kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akipokea Zawadi ya Jogoo wa sikukuu kutoka kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mara baada ya kukutana nao mapema leo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akisaini kitabu cha wageni mapema leo baada ya kukutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...