Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewatahadharisha wafanyabiashara watakaogushi taarifa kwa nia ya kupatiwa vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
Amesema kuwa jukumu lake ni kuvikabidhi kwa wakuu wake wa wilaya ili nao kuvifikisha kwa wakurugenzi na hatimae kuwafikia walengwa wa vitambulisho hivyo na kuongeza kuwa wajasiliamali waondoe shaka juu ya idadi ya vitambulisho hivyo kwani vikiisha vitaagizwa vingine na hakuna atakaekosa.
“20,000/= kwa kila kitambulisho, lakini kwa mtu yeyote yule ambae atakuwa “amefoji” ambae atapewa kitambulisho bila ya kustahili atanyang’anywa kitambulisho hicho na 20,000/= hazitarudi, kwahiyo nitoe angalizo kwa hawa wajasiliamali wadogo wadogo wazingatie hizo taratibu ambazo zimewekwa,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vitambulisho hivyo 25,000, kwa wakuu wa Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi zenye halmashauri nne, hivyo kila halmashauri kupatiwa vitambulisho 6,250.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (Kulia) akikabidhi vitambulisho vya wajasiliamali kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (Kulia) akikabidhi vitambulisho vya wajasiliamali kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akisaini hati ya kupokea vitambulisho kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo muda mfupi kabla ya kupewa vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...