Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Salum Shamte amewataka vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi kutumia fursa inayotolewa na Shirika la Angel Investors (Wawekezaji Malaika) ambalo limekuja nchini kuwafikia Watanzania kwa kutoa mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo ili kupiga hatua.
Shamte ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi maalumu wa ufunguzi wa Ofisi ya Taasisi inayohudumia Vijana ambao ni wavumbuzi, wabunifu wanaoanza biashara ambapo watasaidiwa na Taasisi ya World Business Angel Investment Forum (WBAF) ambayo limejikita kupeleka huduma za kifedha kwa Vijana hao. Aidha Shamte amesema kuwa asilimia kubwa ya vijana hapa nchini wana ukosefu wa ajira pamoja na kupata mtaji wa kujiendeleza katika biashara.
Mkurugenzi Mkazi wa Angel Investors Tanzania (Wawekezaji Malaika), Sabetha Mwambenja amesema kuwa tayari wamesha fanya mazungunzo na Sekta ya Umma na Binafsi ikiwamo Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Tumaini, VETA, COSTECH, Taasisi yaTeknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Kilimo cha Sokoine, (SUA), Chuo cha All Makhoum cha Mbezi Beach na Hatamizi za Tehama (Incubators).
Mkurugenzi
Mkazi wa Angel Investors Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja akifafanua ujio
wa taasisi hiyo wakati wa ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini,
kuwa ni kutaka kuinua Vijana wasomi katika suala zima la kujiajiri kwa
kuwawezesha namna ya kupata mtaji ili kujikwamua kiuchumi wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Sekta Binafsi Tanzania Salum Shamte akisistiza suala la Vijana waso
kutumia fursa inayotolewa na Taasisi ya World Business Angels
Investment Forum (WBAF) lililojikita kutoa huduma za kifedha kwa
Vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi wanaoanza biashara kupiga hatua na
kuwa wafanyabiashara wakubwa, leo katika ufunguzi wa ofisi ya taasisi ya
WBAF Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Biashara na Maendeleo nchini Ghana Ibrahim Awal ambaye pia ni mkulima amehudhuri ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam..
Mkurugenzi Mkazi Angel Investors Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja (kushoto) na Mwenyekiti WBAF Baybars Altuntas (kulia) wakionyesha mafaili kuashiria ufunguzi wa ofisi ya WBAF hapa nchini umeshakamilika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...